Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Abdulwahab al-Safi, mwandishi wa habari wa Iraq, katika mahojiano na tovuti ya habari ya Al-Ahd, amesema: "Bila shaka, iwapo Marekani itafanya tena mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Iraq itakabiliwa na shinikizo kubwa sana. Hata hivyo, serikali ya Iraq na makundi yote ya kisiasa yanayoshiriki katika shughuli za kisiasa nchini humo hayapaswi kusalimu amri mbele ya shinikizo hilo. Aidha, haipaswi kusahau wala kupuuza misimamo ya heshima ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono na kuisaidia Iraq katika nyakati nyingi ngumu ilizopitia huko nyuma.
"Hili ni muhimu hasa baada ya uvamizi wa kundi la kigaidi la Daesh katika miji mingi ya Iraq, wakati wa majira ya joto ya mwaka 2014. Katika kipindi hicho, Iran ilitoa msaada na ushirikiano wa kila aina kwa Iraq, wakati ambapo nchi nyingi zilikwepa kutekeleza wajibu na ahadi zao. Hali hiyo ilidhihirika zaidi kwa Marekani, ambayo ina mkataba wa kiusalama na Iraq."
Ni marufuku kutumia anga ya Iraq kwa ajili ya mashambulizi
Al-Safi amesisitiza kuwa; serikali ya Iraq haipaswi kuruhusu ndege za kivita za Marekani na Israel kutumia anga ya nchi hiyo kufanya mashambulizi dhidi ya Iran au nchi nyingine yoyote.
Maoni yako